Migne

Kocha wa Harambee Stars Sebastain Migne ajiuzulu

Harambee stars sasa italazimika kutafuta huduma za mkufunzi mpya baada ya Sebastian Migne kujiuzulu.

Migne

Minye ambaye aliteuliwa mkufunzi mkuu wa Harambee Stars mwaka 2018 alijuzuku baada ya kufanya mashauriano na shirikisho la soka nchini FKF, taarifa ya shirikisho hilo ilisema.

Migne aliongoza Stars kufuzu kwa dimba la taifa bingwa barani Afrika Afcon baada ya kuwa gizani kwa takriban miaka 15.

Vijana wa taifa walifanikiwa kushindi mechi moja pekee katika dimba hilo kwa kulaza majirani wa Afrika mashariki, Tanzania mabao 3-2. Hata hivyo Kenya ilipoteza mechi zingine za makundi dhidi ya Senegal na Algeria.

Masaibu ya mkufunzi huyo hata hivyo yalianza pale Harambee Stars ilipobanduliwa nje ya kinyang’anyiro cha CHAN na majirapni Tanzania mbele ya maelfu ya mashabiki wa nyumbani.

Francis Kimanzi ambaye amekuwa naibu mkufunzi mkuu anatarajia kushikilia majukumu ya kikosi cha taifa huku mkufunzi wa kudumu akisakwa.

Photo Credits: Star

Read More:

Comments

comments