Konde Boy kutumbuiza jukwaani na Ali Kiba,uhuru wa kutema lebo ya WCB

alikiba-harmonize-696x418
alikiba-harmonize-696x418
Konde Boy na Ali Kiba watakuwa wanaamsha popo Disemba hii katika ukumbi wa Uhuru uliopo jiji kuu la Dar Es Salaam.

Hii itakuwa mara ya kwanza Harmonize kutumbuiza katika jukwaa moja na Ali Kiba kutoka aiteme lebo ya WCB.

Tayari mapromota wa fiesta hiyo washatangaza kuwa mastaa hawa watakuwa katika ukumbi huo.

https://www.instagram.com/p/B5cqKRyhMXT/

Tangazo la fiesta linajiri hii siku chache baada ya Harmonize kumaliza ubishi na mtayarishaji muziki hapa nchini Magix Enga.

Mkwaju huu ulikuwa ushaanza kupata upigwaji mkubwa redioni hapa nchini na kushika nafasi za kwanza katika mtandao wa YouTube.

Ikumbukwe kuwa Harmonize alikuwa amefanya ziara kubwa Afrika mashariki akipigia Uno kampeni kubwa.

Ina maana kuwa meneja wake alifanya mazungumzo na kuridhiana na Magix Enga.

https://www.instagram.com/p/B5a8D78HIhX/

Tukio la mastaa hawa wawili litakuwa la ajabu sana wengi wa mashabiki wakisubiria tamasha la kukata na shoka.

Zamani kipindi na amabapo Konde Boy alikuwa WCB, tamasha kama hili la kukutana na Alikiba halingefanyika.

Kima cha hela alichodaiwa na lebo ya Wasafi ni takriban milioni Tsh 5OO.

Harmonize anatakiwa kulipa hela hiyo ili kupata hatimiliki ya jina na ngoma alizotoa chini ya WCB.