Kongamano la magavana lililotarajiwa kufanyika katika kaunti ya Makueni lafutiliwa mbali

NA NICKSON TOSI

Kongamano la saba la magavana nchini lililotarajiwa kuandaliwa katika kaunti ya Makueni kuanzia Tarehe  20-23 Aprili mwaka huu limefutiliwa mbali  kwa hofu ya Corona.

Kongamano hilo huwaleta pamoja viongozi wa serikali kuu na magavana wa magatuzi yote 47 nchini ili kujadili hatua ambazo serikali hizo za ugatuzi zimeafikia na changamoto ambazo zinakumba ugatuzi nchini.

Jumla ya watu 179 tayari wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona nchini Kenya. Hii sio hafla ya kwanza kufutiliwa mbali kutokana na janga la corona huku ligi mbali mbali za soka duniani zikisitishwa kutokana na hofu ya maambukizi ya corona.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO