Korti ya Abuja ,Nigeria yahalalisha ukahaba nchini humo

Screenshot_from_2019_12_20_16_05_52__1576847173_24861
Screenshot_from_2019_12_20_16_05_52__1576847173_24861
Korti ya Abuja nchini Nigeria imeweka bayana kuwa ukahaba sio tendo la uhalifu kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Uamuzi huo wa kihistoria umefanyika baada ya kesi ya washukiwa wa ukahaba kuwasilishwa mahakamani.

Mila na desturi za kiafrika zimefutilia mbali dhana ya wanawake kuuza miili yao ili kupata fedha.

Hata ingawa vitendo kama hivyo vinafanyika, ni ukiukaji wa sheria katika mataifa mengi Afrika.

Jaji wa mahakama hiyo Binta Nyako amesema kuwa hakuna uwepo wa sheria zinazoharamisha tendo la wanawake kufanya biashara ya ukahaba.

Aidha jaji ameagiza washukiwa hao walipwe fidia baada ya kupatikana kuwa hawana hatia.

Uamuzi kama huu utaathiri maamuzi yajayo ya mahakama kuhusiana na swala hili nchini Nigeria.

Wanawake hao sasa wanataka walipwe fidia kwa sababu za kuaibishwa hadharani, kuibiwa na kupokonywa hela zao.