Kosa uchekwe! Mechi 5 za AFCON zitakazo kusisimua wikendi hii

AFCON (1)
AFCON (1)
Baada ya Kenya kuwa miongoni mwa timu ambazo zilibanduliwa katika kipute cha AFCON wiki hii, raha na vihemko vya mashindano hii zatarajiwa kuongezeka wikendi hii katika mmechi za 16 bora.

Ratba ya mechi za maondoano za AFCON imeshuka na kipute kinaendelea siku ya ijumaa.

Hata hivyo baadhi ya mechi nane ambazo zitapeperushwa kwako kupitia radio jambo, tumekuwekea mechi tano ambazo zitakuwa za kukata na shoka, na ambazi hufai kukosa.

Ijumaa, Julai 5

Uganda vs Senegal

Mechi hii ambayo itasakatwa mida ya saa nne, itakuwa ya kukata na shoka kwani majirani hao wetu watakuwa timu ya tatu kutoka Afrika mashariki kupambana na simba wa Teranga.

Inaaminika kuwa kila shabiki kutoka eneo hili la Afrika atakuwa nyuma ya Uganda Cranes.

Mechii hii inawadia pale ambapo wachezaji wa Uganda waliregelea mazoezi yao baada ya kuahidiwa kwamba watalipa dola elfu 6 zaidi kila mmoja, na nchi yao.

Kikosi hicho kiliwasilia uwanjani kuchelewa siku ya jumatano baada ya kuahidiwa pesa hizo.

Jumamosi, Julai 6

Nigeria vs Cameroon 7PM

Jumamosi pia mashabiki wa soka duniani watakuwa na bahati ya kutazama mechi kali kati ya magwiji wa bara hili, Nigeria ambao ni nambari 3  huku Cameroon ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hili wakiwa nambari 7 katika bara hili.

Jumapili, Julai 7

Madagascar vs DR Congo 7PM

Madagascar ambao wanasakata kipute cha AFCON kwa mara ya kwanza katika historia yao, wamewashangaza wengi kwa mchezo mwema na wa kumezewa mate.

Timu hiyo ambayo inajulikana kama 'Barea' ambao ni nambari 108 duniani, waliwanyuka Nigeria katika mechi yao ya mwisho ya kundi B na kufuzu kama viongozi na alama 7.

Watamenyana na DR Congo ambayo ina wachezaji mashuhuri kama Cedric Bakambu, Yannick Bolasie, Chancel Mbemba na Arthur Masuaku Jumapili mida ya saa moja.

Algeria vs Guinea 10PM

Siku hiyo hiyo, Algeria ambao wana mchezaji gwiji Riyad Mahrez wanatarajiwa kucheka na nyavu za Guinea ambao walikuwa miongoni mwa timu nne ambazo zilifuzu kama 'best losers' katika kundi B.

Jumatatu, Julai 8

Hata baada ya wikendi kufikia tamati, Jumatatu pia kuna mechi mbili tamu ambazo shabiki sugu wa soka ya Afrika hawezi kosa, kwani hata hautakuwa hoja.

Mali vs Ivory Coast 7pm

Mida ya saa moja, staa wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ambaye anamezewa mate na klabu ya Arsenal atakuwa uwanjani kumenyana na ma staa wa Mali Seydou Keita wa AS Roma na Bakary Sako wa Wolverhampton Wanderers.

Ghana vs Tunisia 10PM

Mechi hii ni moja wapo ya mechi ambazo zinatarajiwa zaidi Afrika na duniani kote, kwani baadhi ya timu hizi mbili kuna mataji 5 ya kombe la bara Afrika.

Je washabikia timu gani?