KPL yaandikia CAF barua ya kupinga hatua ya Nick Mwendwa ya kuwapa Gor Mahia Taji

NA NICKSON TOSI

Usimamizi wa ligi kuu nchini KPL sasa wameandikia shirikisho la soka Afrika CAF barua ya kupinga hatua ya FKF kupitia Nick Mwendwa ya kumaliza msimu wa 2019/2020 .

Katika barua  iliyoandikwa na CAF Aprili 26, 2020 kupitia kaimu katibu mkuu Abdelmounaim Bah, ilitaka ligi zote kutoa mipango mahususi ya kumaliza ligi baada ya virusi vya corona kusitisha kila shughuli katika sekta ya michezo.

Licha ya hayo, Nick Mwendwa aliharakisha kuchukua hatua ya kuwakabidhi Gor Mahia ubingwa wa msimu huu kupitia mtandao wake wa kijamii Machi 30. Hatua ambayo imeibua mgawanyiko miongioni mwa washikadau wa soka nchini.

Katika ujumbe mwengine kwa mtandao wake, Mwendwa alitangaza kuwapandisha Nairobi City stars Kwenye ligi kuu ya KPL.

Kupitia mkurugenzi wake Jack Oguda, KPL ilipinga uamuzi huo na kueleza kushangazwa na hatua ya Mwendwa ya kufanya uamuzi huo japo kulikuwa na muda.

“We find FKF’s purported decision to cancel the season to be out of step with your circular dated April 26, 2020 addressed to your Member Association General Secretaries,” Barua iliyoandikwa na Oguda.

KPL aidha imeiarifu CAF kuwa ni wajibu wao kusimamia ligi na si shirikisho na kutaka CAF kutoa uamuzi kwa sababu vilabu nyingi viko katika hali ya ati ati