Kucheswa nayo!!! 'Niko na watoto wawili kwa ndoa, na sio wa bwanangu,' confesses city woman

Kwenye kipindi cha Sema Na Raey, mama wa watoto wawili alipiga simu kuweza kueleza tatizo lake.

Mama yule ameolewa lakini anauhusiano mwingine nje ya ndoa yake. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa watoto wake wawili sio wa mumewe, ila ni wa mpango wa kando.

"Niko na watoto wawili wasichana kwa ndoa na sio wa mzee. Ni wa mpando wa kando.

Mama huyu amekuwa katika ndoa na mzee wake kwa miaka kumi na nne na amekuwa akiwalea hao watoto wawili ambao sio wake.

Pia anaeleza kuwa aliavya mimba moja ambayo ilikuwa ya tatu kwa sababu watoto walifuatana sana na jambo hilo halikumpendeza.

Skiza akimweleza mtangazaji Annitah Raey.