Kufikia sasa wahudumu wa afya 186 wameambukizwa virusi vya corona

Mkurugenzi mkuu wa afya katika wizara ya afya nchini Dkt Patrick Amoth amesema kufikia sasa wahudumu wa afya 186 wameambukizwa virusi hatari vya corona.

Amoth amesema kati ya wahudumu hao, 102 ni wanawake huku wanaume wakiwa 84.

Alitupilia mbali wazo kuwa kati ya watu waliofariki kufikia sasa, miongoni mwao ni wahudumu wa afya.

 “So far no single healthcare worker has died as a result of the pandemic. The latest cases from Shalom hospital we can confirm they are stable and doing very well,” Amoth .

Amesema kutokana na nambari ndogo ya wahudumu wa afya ambao wameambukizwa virusi hivyo kufikia sasa ni kutokana na hatua ya serikali kuboresha vifaa vinavyotumiwa nao katika harakati zao za kukabilina na maambukizi hayo.
Kufikia sasa, Kenya imesajili visa 6,673 vya maabukizi huku idadi ya watu waliopoteza maisha yao ikifikia watu 149.
Ameongezea kuwa wameajiri wahudumu wa afya zaidi ili kukabiliana  na janga lililoko kwa sasa.

“We need to have more health workers who will serve even in post-Covid-19 times,"