Hayo ndio yaliyokuwa maneno ya mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi Jumatatu muda mfupi tu baada ya Kipchumba Murkomen kufurushwa kama kiongozi wa walio wengi katika seneti.
https://twitter.com/MutahiNgunyi/status/1259804842970820608
"Kama nilivyosema hapo awali, huwezi kumnunua mkikuyu, utaweza tu kumkodisha kwa muda.’ Aliandika katika twitter .
"To my friend Murkomen, Pole Sana. I will pray for you. Now you have enough time to dry your greenhorns."
Wakenya wengi walitoa maoni kuhusu hilo huku Murkomen mwenyewe akicheka baada ya Mutahi kumuandikia hayo .
https://twitter.com/LOYDMUTUA/status/1259817889764384771
Murkomen hapo awali alikuwa ameandika katika twitter kwamba bado yupo thabiti .
https://twitter.com/kipmurkomen/status/1259812121715650560
Badaye Murkomen aliwahutubia wanahabari na kukashifu marekebisho ya uongozi wa seneti. Alisema maseneta wengi hawakuhudhuria mkutano wa Ikulu ya Nairobi uliodaiwa kutekeleza mageuzi ya uongozi katika seneti. Murkomen amesema ataendelea kupigania demokrasia huku akishangaa mbona rais Uhuru Kenyatta anawaelekezea viongozi wa Jubilee hamaki .
Ikulu ilitangaza kupitia taarifa kwa wanahabari kwamba seneta wa west Pkot Samule Poghisio ndiye kiongozi mpya wa walio wengi katika seneti. Naibu wake Poghisio atakuwa seneta wa Isiolo Fatuma Dullo Adan. Seneta wa Murang'a Irungu Kang'ata ameichukua nafasi ya seneta wa Nakuru Susan Kihika kama kiranja wa chama cha walio wengi katika seneti. Seneta mteule Farhiya Ali Haji ndiye atakayekuwa naibu wa Kang’ata.