Kulikoni! Zari akanusha madai ya kummezea mate 'Handsome' Sonko

Zari
Zari
Aliyekuwa mpenziwe mwanamziki Diamond, Zari Hassan amepuuzilia mbali madai katika mitandao ya kijamii kwamba anamhemea sana kimapenzi gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Jumatano Zari kupitia ukurasa wake wa Intagram alisema kwamba taarifa zilizokuwa zikizungushwa mitandaoni kwamba damu yake huyeyuka na mtima wake kusimama tisti anapofikiria Sonko ni potovu.

Habari zaidi:

Katika ujumbe wake, Zari anamshtumu Gavana wa Nairobi kwa kusambaza madai ya uongo na kumtaka aache kueneza upuzi huo.

Habari zaidi:

“Huu upuzi wa huyu mwanamume unafaa kusitishwa. Hapana, sivutuwi hata kidogo nawe, sijawahi kukutana nawe kamwe. Tafadhali achana nami. Wewe sio hulka yangu,” Ujumbe huo ulisoma.

Katika taarifa hiyo, mlimbwende huyo wa mitindo raia wa Uganda aliripotiwa kummezea mate ‘handsome Sonko’ na kutamani kukutana naye mwishoni mwa mwaka huu.