Kumbukumbu na mafanikio makuu ya marehemu Rais Moi

Moi
Moi
Alipochukua hatamu za uongozi kutoka kwa Mzee Jomo Kenyatta, Rais Moi aliahidi kufuata Nyayo zake katika uongozi wake.

Rais mstaafu Daniel Moi alitawala Kenya kwa miaka 24,  alichukua hatamu ya uongozi kutoka kwa Rais wa kwanza wa Kenya marehemu Jomo Kenyatta ambaye aliaga dunia Agosti  1978 katika Ikulu ya Mombasa.

Huku tukiendelea kumkumbuka mzee Moi, leo tunajikumbusha zaidi kuhusu utawala wake kwani alifahamika kutokana na ukakamvu wake kisiasa ambao wakosoaji wake wanasema ulikandamiza uhuru wa Wakenya.

Hata hivyo, wachanganuzi wa kisiasa wanasema kwamba uongozi wake ulikuwa wa aina yake na bora zaidi ikilinganishwa na jinsi mambo yalivyo sasa.

Usalama wa Nchi

Katika uongozi wake usalama ulikuwa ni dhabiti sana. Hakukuwa na vitisho kutoka kwa makundi hatari yanayoangaisha raia kama vile tunavyoshuhudia katika mitaa ya Nairobi na hata katika sehemu toafauti za nchi. Ijapokuwa kulitokea mashambulizi ya kigaidi katika Hoteli ya Norfolk na katika ofisi za balozi wa Marekani, utawala wa Moi ujizatiti sana kukabiliana na ukosefu wa usalama.

Kashfa za Ufisadi

Ijapokuwa kulikuwa na kesi chache za ufisadi hususan za Goldenburg. Tuna imani kwamba utawala wake haungekuwa ilivyo sasa. Jinsi tunavyoshuhudia sasa ni ufisadi katika kila wizara au kila ofisi ya serikali intuhumiwa kwa kashfa.

Matatizo ya mipaka za nchi

Rais mstaafu Moi anakumbukwa kuwa asiyetia mzaha katika masuala ya mipaka ya taifa hili. Hivi sasa Kenya inakumbwa na matatizo ya kimipaka na majirani. Hivi majuzi kumeibuka mzozo wa kimaeneo baina ya Kenya na Uganda katika kisiwa cha Migingo. Kwa sasa Kenya inazozania eneo la Bahari Hindi na nchi Somalia.

Hatua ambayo imesababisha nchi hizi mbili kuwasilisha kesi katika mahakama kuu ya kimataifa.

Malumbano ya Kisiasa

Rais Moi anakumbukwa kwa kupinga kila njia siasa za matusi na malumbano za kila mara. "Siasa mbaya, Maisha Mbaya" Ni tamko ambalo profesa huyo wa siasa alipenda sana kusema akinuia kuwaonya wanasiasa waliojibizana nao hadharani.

Tuzo kwa Wanaspoti

Katika kila halfa iliyoadmishwa, Moi hangekosa kuwatambua wale waliotia fora katika nyanja tofauti tofauti kimichezo. Isitoshe rais mstaafu alijizatiti na kujenga viwanja kadhaa vya kimichezo vikiwemo Nyayo Stadium na Moi International Sports  Center Kasarani.

Maziwa ya Nyayo kwa shule

Wengi wanakumbuka Maziwa ya Nyayo ambayo ilikuwa ni kivutio maalum cha kwenda shule haswa kwa wanafunzi waliotoka katika maeneo kame. Moi alikuwa na hari ya vijana wote kupata elimu ndiposa akajenga vituo vingi vya kielimu pamoja na shule nyingi za msingi na sekondari.