Kunani? Ken Walibora ndiye mwanahabari wa tatu kupoteza maisha yake kwa kugongwa na matatu

Mwenda zake profesa Ken walibora aliaga dunia kwa kugongwa na matatu na mwili wake ulipatikana katika chumba ha kuhifadhi maiti cha Kenyatta baada ya kupotea Ijumaa ya siku ya pasaka.

Ilisemekana kuwa Walibora aligongwa na matatu siku ambayo alipotea.

"AT THE TIME HE NOT DRIVING. ON HIM WAS FOUND A MERCEDES BENZ CAR KEY AND PRESS CARD IN HIS POCKET. AND A PRESS CARD.”

Mwendazake Walibora alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Riara, familia bado haijapeana ratiba ya mazishi ya mwendaazake.

Si Walibora pekee ambaye alihusika katika ajali ya kugongwa na matatu;

Kwa muda wa miezi miwili, wanahabari wawili wa runinga ya NTV waligongwa na gari kisha kupoteza maisha.

Christine Omulando, 46, ambaye alikuwa mhariri aliripotiwa kupotea baada ya familia, marafiki kumpigia simu na kumkosa.

Aliripoti kazini Jumatatu, machi, 16 na kutoka ofisini adhuhuri, polisi walisema kuwa gari liligonga watu na miongoni mwa waliogongwa alikuwa Christine.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Khoja Nairobi, christine aliaga dunia papo hapo.

Kifo kingine kilikuwa cha mhariri Raphael Nzioki ambaye aligongwa na matatu kisha likatoweka mapema mwezi wa machi.

Nzioki alipata ajali katika eneo la Kenyatta Avenue, Kimathi street.

Polisi walithibitisha kisa hicho na kusema kuwa gari hilo liko mikononi mwa polisi.