Wizara ya afya imechukua hatua hiyo ili kupambana na ufisadi na sasa kituo cha huduma za Maabara kwa umma, Kenyatta National Hospital (KNH) na shirika la utafiti wa matibabu KEMRI haziruhusiwi tena kupima corona.
Memo iliyotolewa kwa wakuu wa vitengo mbalimbali imeonyesha pia kwamba hospitali ya Mbagathi iliyokuwa ikitumiwa pia kufanya vipimo sasa haitawachukua watu wanaoshukiwa kuwa virusi hivyo bali itawalaza tu wale ambao tayari wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona.
Kemri, kwa upande wake imetangaza kwamba haitakuwa ikikusanya sampuli za covid 19 na badala yake itakuwa ikizipima sampuli kutoka vituo maalum vilivyopewa idhini ya kuchukua sampuli.
Wakenya sasa watategemea makundi maalum ya dharura yatakayokusanya sampuli kutoka kwa mashirika na vituo maalum ambayo yatataka huduma za kupimwa na kuwekwa katika karantini.