Kuna tofauti ya kuitwa baba na kuwa baba-Jacque Maribe

Jacque Maribe ni mwanahabari ambaye anajulikana sana nchini Kenya kwa sababu ya taaluma yake ya uanahabari lakini jina lake lilipaa sana kutokana na kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani.

Jacque ni mama wa mtoto mmoja wa kiume na alisema kwamba anajivunia kuwa mama.

Huku akimlimbikizia sifa mchezaji gwiji wa mpira wa vikapu marehemu Kobe Bryant, Maribe alisema kwamba alipenda sana uweledi na ubunifu wa Kobe kusakata mpira wa kikapu.

" Nimekua nikimjua Kobe kwa sababu ya upendo wake wa mchezo wa mpira wa Vikapu, upendo wake kwa familia yake na pia kwa mwanawe Gianna,

"Singecheza mchezo huo kwa maana nilikua mfupi," Aliandika Maribe.

Aliendelea kusema kuwa kama vile Gianna alikuwa mtoto wa baba pia yeye anajivunia kuwa mtoto wa baba.

" Nimekuwa tangu utotoni "mtoto wa baba" na najivunia kuwa mtoto wa baba, si mimi peke yangu pia dada zangu wawili ni "watoto wa baba,"

"Pia najivunia kuwa mama wa mvulana mmoja ambaye ana sura ya kupendeza," Jacque alisema.

Kupitia akaunti yake ya instagram alisema kuwa mengi yanasemwa na yataendelea kusemwa lakini anajua kuna tofauti kubwa ya kuitwa baba na kua baba.

"Mengi husemwa lakini ambacho najua kuna tofauti ya kuitwa ba kuwa baba,

"Baba ya kumzaa mtoto na baba ambaye ameamua kukaa katika maisha ya mtoto, baba ambaye anaamua kumlisha mtoto,msaidia katika kazi yake ya ziada,

"Na hata kuenda kucheza na yeye," Alieleza.

Aliandika pia na kusema kuwa anawasherehekea wanaume ambao si baba wa kumzaa mtoto lakini aliamua kukaa na mwanawe kumlea na kumpongeza babake kwa kumlea.

"Nataka kusherehekea baba yangu kwa kunilea na pia wanaume ambao wanawalea watoto ambao si wao kuwazaa,

"Na nitazidi kuwapenda na kuwasherehea kwa kitendo hicho,"