Kundi la wabunge wachanga waratibiwa kukutana na Rais Kenyatta

wabunge.wachanga
wabunge.wachanga
Kundi la wabunge wachanga KYPA wakiongozwa na Mwenyekiti Johnson Sakaja wameratibiwa kukutana na Rais Uhuru kenyatta kujadili masuala yanayoadhiri maelfu ya vijana nchini.

Akiongea katika hafla ya pamoja iliyoandaliwa katika hoteli moja hapa Nairobi kuwatunuku wabunge walioshiriki mafunzo kuhusu uongozi bora chini ya programu ya Leading Young, Sakaja amewataka wabunge hao kumakinika uongozini.

Matamshi ya Sakaja hata hivyo yameungwa mkono na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino aliyepia katibu wa muungano huo akiwataka wabunge kuwajibikia majukumu yao.