- Murathe awali amesema Uhuru atasalia uongozini ingawa katika wadhfa tofauti .
- Kuria amesema Rais anaweza kujizungumzia na hawezi kuwatumia ‘walevi’ kufikisha ujumbe wake .
Siasa za mwaka wa 2022 sasa zimechukua mjadala mpya baada ya kuibuka hoja ya iwapo rais Uhuru Kenyatta ataondoka madarakani wakati kipindi chake kuhudumu kitakapofika tamati mwaka huo .Jana katika maazishi ya mamake mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ,naibu wa rais William Ruto alionekana kutoa matamshi ya kuondoa kabisa mpango wowote wa rais kusalia uongozini kwa kusemakwamba rais Kenyatta ni Mtu mungwana na hatobadilisha katiba ili kusalia uongozini . Hatua hiyo yake sasa pia imewafanya viongozi wengine kuanza kutoa kibwagizo hicho huku mbunge wa gatundu Kusini Moses Kuria akikariri kauli hiyo kwamba kamwe rais Kenyatta hana mpango wa kuendelea kuongoza baada ya hatamu yake kukamilika katika miaka miwili ijayo.
Kuria pia aliyesema hayo wakati wa hafla hiyo ya kumzika Martha Kirigo, mamake mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua na aliyekuwa gavana wa Nyeri marehemu Nderitu Gachagua. Mbunge huyo wa gatundu kusini aliwataka waomboleza kumpuuza aliyekuwa naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe ambaye maajuzi amedai kwamba rais atasaliamadarakani hata baada ya mwaka wa 2022 katika wadhfa mwingine wenye ushawishi .
Hofu za kuwepo mpango wa rais kusalia madarakani baada ya 2022 ndizo zinazozua pingamizi na maswali kuhusu nia ya rais Kenyatta na kiongozi wa odm Raila Odinga hasa kuhusiana na jopo la BBI na mapendekezo yaliyotolewa na Jopokazi hilo . Kuria alimtaja Murathe kama ‘mlevi’ ambaye walikuwa wakinywa naye pombe hadi mwaka huu alipoamua kuacha pombe ."Mimi nimewacha pombe mwaka huu lakini hiyo miaka mingine tulikua tunakunywa na Murathe’. Kuria alisema .