Burale

Kushiriki mapenzi na watu wengi haikufanyi mwanaume – Burale

Mhubiri Robert Burale alifunguka na kusema kuwa, kushiriki katika tendo la ndoa na watu wengi hakumfanyi kijana kuwa mwanaume kama vile vijana wengi hujigamba.

Burale aliwashauri vijana wangoje mpaka watakapo pata bibi ndipo washiriki kimapenzi na wapendwa wao.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Burale alisema kuwa, vijana wengi huona haya  kuzungumzia mada ya ngono lakini ni muhimu sana kwani haya ndio maswala ibuka yanayowachanganya sana vijana.

Malimwengu haya! Jamaa amzika kuku na kusoma bibilia kaburini mwake

Vilevile, Burale alisema kuwa, kushikiriki kimapenzi mapema hufanya uhusiano wako na Mungu uende chini kila wakati unaposhiriki kwenye tendo hilo.

Licha ya hayo, Robert alilizidi kusisitiza kuwa, kushikriki ngono na watu wengi huwa haimfanyi kijana kuwa mwanaume bali humfanya kijana huyo kuwa kijana tu, mwenye umbo la mwanaume.

Zaidi ya hayo, aliwambia vijana, huenda wakawa wanajivunia sasa hivi kwa vitendo wanavyofanya lakini itafika wakati ambao wanawake watataka mume wa kuoa na si kijana barobaro tu, mwenye umbo zuri.

Taharuki kuhusu ongezeko la visa vya mimba za wasichana wadogo Murang’a

      “Do not give away your destiny and strength. You got to understand you may be bungling with these sexual            activities right now and think that every woman is excited by you because you have a six-pack but when the            time comes women will not look for sex partner perse but a real man to marry.”

Mwisho kabisa, alisema kuwa, hawa wanaume huenda wakawa wanaume wenye umbo nzuri sana,magwiji kitandani lakini hawana wa kuwasifu.

 

Photo Credits: Douglas Okiddy

Read More:

Comments

comments