'Kusonga juu na kuendelea,' Serah Teshna asema baada ya kuacha kazi K24

Serah Teshna hatimaye amewacha jukumu lake la ushirikishi katika onyesho la asubuhi, Alfajiri, kwenye chaneli ya K24.

Ijumaa tarehe thelathini na moja ilikuwa siku yake ya mwisho kushirikisha onyesho hilo.

Alielekea Twitter kusema kwaheri. Serah aliwashukuru wanzilishaji wake, wakurugenzi na familia yote ya MediaMax ambayo ilifanikisha onyesho lake tangu ajiunge, tarehe kumi na tatu mwezi wa Novemba mwaka wa elfu mbili na saba.

Hata hivyo si wazi pahali ambapo anaelekea, lakini kituo hicho chadai kuwa alitaka kuweka makini kwa kucheza.

''Asanti @SerahTeshna, milele utakuwa sehemu ya #AlfajiriFam,'' ilisoma mtandao ya twita ya K24, ikiendelea, ''#AlfajiriFam, tumpongeze @SerahTeshna kwa kuwa bora kwenye E-nteractive kila siku ya juma kutoka saa moja hadi saa moja unusu katika #K24Alfajiri. Tutakukosa!''

'Kusonga juu na kuendelea,' Serah Teshna asema baada ya kuacha kazi K24

Kwenye twita Serah aliandika:

''Ni onyesho langu la mwisho kabisa la Alfajiri katika K24Tv na nataka muniunge kwa vile itakuwa 🔥 🔥 #K24Alfajiri.''

Aliongezea zaidi huku akigusia mashabiki wake:

''Asanti kwa kuniunga mkono. Inamaana kubwa sana kwangu. Kusonga juu na kuendelea mbele 🙏🏾🙌🏽”

Mashabiki wake waliosikitika walijibu posti yake. Soma baadhi ya walivyosema

Brian Andrew: @SerahTeshna Missing you already 😢. You’ve done a good job and spiced up our mornings To the next chapter, I still got your back. Wish you good luck. 🙌

Shiksha Arora: Good luck my dear @SerahTeshna will miss you at @K24Tv #Alfajiri😘❤️💕 You’ll forever be my favourite!

AG_Nyangaresi: Aaaye!…I don’t know how the mornings are going to be without waking up to you on TV. But i bet you on to something bigger and better. You go girl!

Tadeo David: It was heartbreaking to watch you for the last time on the show. I shall miss you.. You would brighten my mornings on the show… But wish you all the best on your next step.. Always forward, never backwards.

Williemarigi: How everyone is pretending to be ok…

Kama zawadi ya kwaheri kwa mashabiki wake, tazama baadhi ya picha za Serah akionyesha uhodari wake wa mitindo wa mavazi.