Mtaalam wa kupambana na ugaidi Jane Mariott ndiye balozi ajaye wa Uingereza humu nchini kuanzia septemba mwaka huu . Ataichukua nafasi ya Nic Hailey ambaye amekuwa nchini tangu mwaka wa 2015 . Mariott mwenye umri wa miaka 43 atakuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa balozi wa Uingereza humu nchini.
Bi.Mariott amewahi kuwa balozi wa Uingereza nchini Yemen kati ya mwaka wa 2013-2015 na maajuzi amekuwa mkurugenzi wa Kituo cha kimataifa cha kupambana na ugaidi . Pia amewahi kuhudumu kama mshauri wa Richard Holbrooke aliyekuwa mjumbe maalum wa uingereza katika mataifa ya Pakistan na Afganistan .
Katika ujumbe wake kwenye Twitter amesema amefurahia sana uteuzi wake kuja Kenya na atafanya kila juhudi kuboresha uhusiano kati ya Kenya na Uingereza .