kutoka kwa Jaguar hadi kwa Gloria Muliro,'Wasanii waliohudhuria ibada ya Papa Dennis

Papa-Dennis-696x870
Papa-Dennis-696x870
Wasanii tofauti wamejiunga na familia na marafiki wa mwendazake Papa Dennis katika ibada yake ilioandaliwa eneo katika kanisa la Nairobi chapel baada ya mwanamziki huy kufariki wiki mbili zilizopita katika njia tatanishi.

Ibada hiyo ya wafu iliweka ili kusherehekea maisha ya Papa ambaye mwili wake ulipatika Pangani 08/02/2020.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria ibada hiyo ni;

1. Gloria Muliro – msanii wa nyimbo za injili

2. DK Kwenye beat – msanii wa nyimbo za injili

3. Ringtone – msanii wa nyimbo za injili

4. Mwenye Haki

5. Kevochi

6. DJ Euphoric

7. Gabu wa P Unit – msanii wa nyimbo

8. Jaguar – mbunge wa Starehe

Awali pacha wake Papa Dennis alisimulia jinsi alikuwa na Papa kabla ya kukumbana na kifo chake usiki huo.

“Nilikua na Papa Dennis mtaa wa Jamhuri siku ya ijumaa, kutoka hapo alienda Pangani, baada ya muda niliungana naye mwendo wa saa tatu usiku kwa sababu alikua ameniambia nmpelekee paspoti yake.” Alieleza Simon.

Aliongeza na kusema,

“Baada ya kumaliza kuwasalimia na kuongea mambo tofauti, nilienda kumtafuta ndugu yangu, nilienda katika kijumba cha kurekodi,msalani,jikoni lakini sikumpata Papa.” Alizungumza.

Baada ya hapo waliarifiwa kuwa kuna mwili ambao umepatikana nje ya jumba hilo na ulikuwa unafanana na msanii papa Dennis.

“Tulithibitisha kuwa mwili huo ulikua wa ndugu yangu Papa Dennis, lakini wakati huo hakua amekata roho, tulipigia huduma za ambyulensi tofauti lakini nguvu zetu ziliambulia patupu kwa sababuilichukua muda kupokea simu

Tuliona ambyulensi iliokua imepita karibu na tukio tukasimamisha lakini haikusimama, tuliona ya pili ambayo ilisimama lakini madaktari walipomchukua waliniambia Papa Dennis ndugu yangu amekata roho.” Simon Alieleza.

Pacha huyo amewatumbuiza watu ambao walikuwa katika ibada hiyo huku akiimba nyimbo tofauti alizokuwa ameimba nduguye Dennis.