kanyari1

Kutokomaa kulinigharimu ndoa yangu, asema Kanyari.

Mhubiri tata Victor Knyar8i hatimaye ameelize kile kilichosababisha ndoa yake na mwanamziki maarufu Betty Bayo kuvunjika.

Akizungumza na gazeti la The Star siku ya Jumamosi, Kanyari alisema kuwa walioana wakiwa bado ni wadogo na hawajakomaa. “Betty was the best woman I have ever met but I think when we met we were both still childish, I was only 31 years.”

Hiyo ndiyo sababu kuu iliyopelekea ndoa yetu kuvunjika manake Betty hakuwa mwanamke mbaya, anaweza kuwa na maoni yake ya ni kwanini ndoa yetu haikufaulu lakini kutokomaa kulichangia pakubwa.

Kanyari aliendelea na kusema kuwa hakuwa wamekomaa visawa kiakili kuweza  kustahimili ndoa lakini sasa wamekomaa na wanaweza kuchagua ni kipi kinachowafaa.

kanyari3

Wengi wanaamini kwamba wawili hao walitengana baada ya Betty kugundua kwamba mumewe amekua akieneza injili ya uwongo, lakini Kanyari anasema si kweli. Anasema kuwa ufichuzi uliopeperushwa katika runinga moja nchini haikuwa sababu ya wao kuachana kwa sababu alisimama naye wakati huo wote.

Kanyari anasema kuwa hakuwa tayari kuyatilia maanani aliyohimizwa na mkewe, kama vile kufika nyumbani mapema jambo lililopelekea wao kuzozana mara kwa mara.

 

Alipouliza kama anampenda Betty, alisema kuwa hawezi kusema ndio au la.

 “You cannot force love to anyone. Na ukiachwa achika. I would say, if she loves me, I love her too but if she does not, then why should I force myself to her? If you are mature enough you let things unfold themselves without forcing them to happen because it could affect both of us. Love is a journey, and I loved her then but for now, I don’t know what her heart has.”

Hata hivyo Betty ameendelea na maisha yake na atafunga harusi tena hivi karibuni.

 Alisema Kanyari:

“The time will come for me to move on and the whole world will know but for now no hurry in Africa. I will move on when I want, let me have my good time and continue serving God,” 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments