Viongozi wa upinzani Zimbabwe waliokuwa wametoweka wamepatikana wakiwa wamepigwa vibaya

MP-JOANA-MAMOMBE-730x414
MP-JOANA-MAMOMBE-730x414
Baada ya taarifa kujiri kuhusiana na kutoweka kwa wabunge wa upinzani Zimbabwe, imebainika kuwa wabunge hao watatu wa chama cha MDC wamepatikana kama wamepigwa na kuachwa na majeraha mabaya  kando ya barabara. Taarifa ambazo zimethibitishwa na chama hicho.

MP Joanna Mamombe, kiongozi wa Vijana  Cecilia Chimbiri na  Netsai Marov walisemekana kutoweka katika njia tatanishi baada ya kuandaa maandamano Jumatano kuhusiana na jinsi serikali inavyolichukulia swala la Corona.

Maandamano hayo aidha yalipinga hatua ya serikali kulifunga taifa hilo huku wananchi wengi wakiendelea kufariki kutokana na njaa.

Chama cha MDC kupitia kurasa zake za mitandaoni kimesema kuwa viongozi hao watatu wamepelekwa hospitalini.

Taifa la Zimbabwe limeshutumiwa na mataifa ya Marekani na Uingereza kuhusiana na dhuluma ambazo viongozi wa upinzani wa taifa wamekuwa wakipitia siku za hivi karibuni.