'Kwa uwezo wa Mungu itarudi,'Hisia za Harmonize baada ya kibao cha Diamond kutolewa youtube

zuchu
zuchu
Baada ya kibao chao Diamond na Zuchu kupokelewa vyema na wanamitandao na mashabiki wamepata pigo kubwa baada ya kibao chao cha 'cheche' Kutolewa kwenye youtube.

Siku tatu baada ya kibao hicho kimetazamwa na watazamaji millioni 2.4, si mara ya kwanza msanii Diamond kudaiwa kuiba mitindo ya wasanii wenzake bali ni mara kadhaa endapo atatoa kibao kipya na kupokelewa vyema na watazamaji.

Aliyekuwa msajiliwa wa lebo ya WCB Harmonize alichukulia jambo hilo kwa uzima hii ni baada mmoja wa mashabiki wake kumwambia kuhusu kutolewa kwa kibao hicho kwenye youtube.

Msanii huyo aliyefahamika kama aucho bill alikuwa na haya ya kumwambia Harmonize;

"Video ya cheche huko kwa wazee waku copy."

Kwa haraka Harmonize alikuwa na haya ya kumjibu;

"@aucho bill sasakilichokufurahisha nini mpaka ulete hizi habari kwa shamra shamra...?? au ulihisi ndio utanifurahisha Ajali kazini ku copy ni kawaida Hasa ukiwa umefanya mambo mengi ubongo ni kawaida kujaa...kwa uzo wa Mungu itarudi tuhurumiane Ili tuone pepo ya Mungu..!!!! one love." Alijibu Harmonize.

Diamond na Zuchu walidaiwa kuiba mitindo ya kibao hicho kutoka kwa msanii Beyonce katika kibao chake kilicho fahamika kama 'Naughty Girl'.

Je shabiki huyo alidhani kuwa Harmonize atafurahia kitendo hicho?