KWALE: Wanafunzi wapewa dawa za uzazi wa mpango kuzuia mimba

Mimba za utotoni zinachangia 25% ya wasichana kuacha shule katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Saharan Barani Afrika kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia idadi ya watu UNFPA.

Nchini Kenya wasichana 2 kati ya kila wasichana 10 walio na miaka kati ya 15-19 wanaripotiwa kuwa wajawazito au tayari wamejifungua watoto.

Maeneo yalio na idadi kubwa ya mimba za utotoni ni majimbo ya Narok na Kwale Pwani ya Kenya.

Katika eneo la Kwale wazazi wamelazimika kuwapatia mabinti zao wadogo wengine hadi miaka 10 dawa za kupanga uzazi, ili kuwazia wasipate mimba wakiwa shuleni.

Maafisa wa polisi wa kituo cha Webuye wanamuzuilia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 36 aliyemuua mumewe baada ya mzozo wa kinyumbani.

Babra simiyu kutoka kijiji cha Kibisi eneo bunge la Tongren huko Bungoma anadaiwa kumuua Ronald Simiyu 38 kwa kumpiga na rungu kichwani alipofika nyumbani akiwa mlevi na kumukanyaga mwanao kimakosa.

Babra aidha alikuwa amelalama kwamba Simiyu alikuwa amemuibia shilingi elfu moja na kwenda kulewa nazo.

Majirani walifika na kujaribu kumkimbiza hosipitalini Simiyu kwa kutumia pikipiki na akasemekana kuwa amefraiki baada ya kufika hospitalini