Kwani ni mapacha? Kutana na Andrew, nduguye Bramwell Mwololo

Kwa miaka mingi tumeburudishwa na utangazaji wake Bramwell Mwololo anayetambulika kwa ustadi wake katika kipindi cha mazungumzo wazi wazi.

Kitu ambacho wengi hawajui ni kuwa Bramwell ana ndugu kwa jina Andrew Mwololo ambaye wanafanana kama shilingi kwa ya pili.
Familia hii ya Mwololo imebarikiwa na talanta chungu nzima kwani Bramwell alianzia kama mchezaji wa kabumbu na pia aliwahi cheza raga ya kulipwa.
Andrew naye ana kipaji cha uimbaji kwani yumo katika kwaya ya kanisa la Christ is the answer ministry, Karen.
Kwaya hiyo ilikuwa mojawapo ya vikundi ambavyo viliwatumbuiza wageni katika mkutano wa maombi ya kitaifa wiki iliyopita, katika hoteli ya Safari park.