babu.owino.

Kwani ni mhenga? Tunaangazia nukuu 10 bora zake Babu Owino

Mbunge wa Embakasi mashariki, Babu Owino ni miongoni mwa viongozi wachanga zaidi sio Kenya pekee bali katika kanda hii ya Afrika.

Nyota yake Owino ilianza kung’aa enzi zile akiwa bado kiongozi wa chuo kikuu cha Nairobi, alikopata umaarufu mwingi miongoni mwa wanafunzi na pia wenyeji wa Nairobi.

Ndoto yake ya kuwa kiongozi ilitimia pindi tu alipojiunga na chama cha ODM na kutangaza kuwania kiti cha ubunge kwa mara ya kwanza ambapo alichaguliwa kwa ujumla wa zaidi ya kura elfu arobaine na sita.

Uongozi wake umekuwa wa kuangaziwa sana haswa bungeni kwani ukakamavu na ujasiri wake huonekana kila siku haswa anapotoa hoja zake. Isitoshe mtindo wake wa uongozi ni wa kipekee na ishara kuwa ni mtu anayependwa na watu wake.

Babu Owino pia huangaziwa zaidi ifikapo ni mambo ya kimitindo na ikilinganishwa na jinsi viongozi wenzake huvalia. Awe anavalia suti akielekea bungeni au nguo za kawaida anapotangamana na watu, staili na taste yake ni ya kipekee.

Kingine anachojulikana nacho Owino, ni jinsi anavyochagua maneno yake anapohotubia umati au pia kila anapochapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.

Sio mara moja amejipata matatani kwa kuyatumia maneno ambayo yanakisiwa kuwa ya kuchochea raia.

Hata hivyo, Owino ana hekima na ujuzi wa kujua jinsi ya kuwachangamsha na kuwaacha wananchi wakibubujikwa na machozi kwa ucheshi wake.

Unapopitia mtandao wake wa kijamii, kama sio mambo ya kuuza sera au kuonesha picha za familia yake, Owino mara kwa mara hutumia misemo au methali ambazo huwaacha wengi wakikuna vichwa vyao.

Misemo ambayo hutumia ni ile iliyotumika na bado hutumika sasa katika nchi kadha wa kadha barani Afrika, na hamna anayekaribia kufananishwa naye.

Leo tumekuandalia orodha ya misemo au nukuu kumi bora ambayo amewahi tumia, haswa kwa mtandao wake wa Instagram.

1. A hungry dog licks its private parts while a satisfied dog licks its nose…Kibra Tibim 🔥 🔥

2. No matter how rich you are,no matter how fat your bank account is,no matter what car you drive,no matter how big your house is,no matter how powerful you are,always be humble coz in the end you will leave with nothing and our graves will be the same size.
https://www.instagram.com/p/B2UfFeIHxKH/

3. If you sleep with an itchy ass you wake up with smelly fingers

4. I have no time for tooth paste tooth brush issues.No time for talented time wasters and village salads

5. Everyone wants to join politics.#power is sweeter than orgasm

6. The death of a lion can never be announced by a goat.

7. You want to kiss a girl kiss a book,you want to kiss a boy kiss a pen.To our pupils

8. Gifts make slaves and whips make dogs

View this post on Instagram

Gifts make slaves and whips make dogs

A post shared by Hon.Babu Owino (@he.babuowino) on

9. When a lady has beauty without brains,private parts suffer the most

10. Not all advice from the old people should be listened to.Remember foolish grow old too

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments