Kweli aligharamika! Picha ya pete ya mke wake Nyashinski

nyashinski
nyashinski

Zipporah Bett, mke mtarajiwa wa mwanamuziki Nyashinski ana ujumbe kwa walio na kijicho.

Binti huyu mwenye duka la nguo freshi ameongea kwa mara ya kwanza tangu mume wake mtarajiwa alienda kwao Nandi kwa sherehe za kulipa mahari.

Kwa sasa ni dhahiri kuwa mpenzi wake Nyashinski ndiye atakayemuoa kwani alimvisha pete ya kumchumbia.

Hivi leo, kidosho huyu aliweka picha yake kwenye mtandao wa kijamii na kuandika

‘BET YOU CAN HEAR MY LAUGH FROM THERE…’

Amini usiamini, sadiki usisadiki ni wazi kuwa mwanamziki Nyashinski aligharamika si kidogo alipokuwa akinunua pete hii.