Kwenda Kabisa! Ufisadi peleka uko. KRA yamtimua Kevin Safari

NA NICKSON TOSI

Baada ya mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA kuwa chini ya shinikizo kutoka kwa wananchi kutokana na wafanyakazi wake wanaohudumu mipakani mwa taifa la Kenya na mataifa mengine kuwa fisadi, hii leo mamlaka hiyo imeamua kumtimua afisini mmoja wa waratibu wa mipango Kevin Safari ambaye anakumbwa na madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya afisi.

Nafasi yake imechukuliwa na Pamela Ahago atakayeshikilkia wadhifa huo.

Siku za hivi karibuni,  mamlaka hiyo imekuwa ikisajili hasara kutokana na baadhi ya maafisa wake kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya afisi na ufisadi.