Labda uwache kuwa na umama ndio uwe rais! Bahati asema anaweza piga marufuku mtandao wa Twitter akiwa rais

NA NICKSON TOSI

Twitter ndio mtandao ambao naweza piga marufuku mara yangu ya kwanza nikiwa rais. Ni maoni ya msanii Bahati ambaye alikuwa anawajibu wanaomwingilia kila mara katika mtandao huo kutokana na kile amekitaja ni kuonewa.

Wiki moja tu baada ya kufunga lebo yake ya EMB baada ya kukosana na kila msanii aliyekuwa anafanya kazi chini ya lebo hiyo, Bahati ameanza kuibua mipango yake ya mbeleni.

Jumatatu jioni, Bahati alidai kuwa wakati mmoja atakuwa kiongozi wa taifa hili na kuwataka wale wanaomzungumzia vibaya kuwa na heshima kwake.

“I will be a President of this country one day, so address me with some respect, Mr. Bahati” alisema Bahati.

Usemi huo wake unajiri siku kadhaa tu baada ya kukashifiwa kwenye mitandao ya kijamii na wakenya kutokana na hatua yake ya kuvalia nguo ya mkewe na kurekodi video akicheza wimbo wake mpya akimshirikisha Akothee kwa jina Nakupa Moyo.