Lacazette huenda akahamia Atletico Madrid huku Lemar akijiunga na Gunners

lemar
lemar
Mshambulizi wa Arsenal Alexandre Lacazette huenda akasajiliwa na Atletico Madrid iwapo watashindwa kumsajili Edison Cavani wa Paris Saint-Germain. Afisa mkuu wa Atletico Miguel Angel Gil Marin alikutana na rais wa PSG Nasser Al Khelaifi jijini Paris jana kujadili uhamisho wa Cavani uliopendekezwa.

Mkataba wowote kati ya Arsenal na Atletico unaomhusisha Lacazette kuhamia Uhispania una maana pia huenda kiungo wa Ufaransa Thomas Lemar akahamia Emirates. Lemar amekua na wakati mgumu tangia kuhamia Madrid kutoka Monaco msimu uliopita.

Liverpool wamepigwa jeki na kuregea kwa Fabinho kwenye mazoezi,  na huenda akacheza katika mechi yao dhidi ya Manchester United wikendi ijayo. Raia huyo wa Brazil amekua nje na jeraha la mguu kwa wiki sita lakini sasa amekamilisha matibabu yake na amekua akifanya mazoezi kwa siku kumi zilizopita. Amesema pia sasa yuko tayari kujiunga na mazoezi kamili na kikosi cha kwanza ili aweze kuregea kucheza.

Shirikisho la FKF jana lilizindua Betways kama mfadhili wao mpya wa kombe la Betways FKF kwa mkataba wa miaka mitatu kwa kitita cha shilingi milioni 45.

Mabingwa Bandari wataanza kutetea taji lao kwa mchuano dhidi ya KSG Ogopa FC  katika raundi ya 32. Katika droo hio Gor Mahia watapambana na mshindi kati ya Kariobangi Sharks 'B' na Naivas FC, huku mahasimu wao AFC Leopards wakipambana na mshindi kati ya Elimu FC na KUSCO.

Zoo Youth watapambana na Sindo United huku mshindi akikabana na KCB.

Rais wa FKF Nick Mwendwa anasema ufadhili huo umekuja kwa wakati ufaao na utaboresha soka mashinani. Ufadhili huu unajiri baada ya kampuni ya Sportpesa kujiondoa kutokana na kile walichokitaja kuwa kutozwa ushuru wa juu mno.