Lady Maureen yuko hai-Akothee aweka mambo wazi

Mashabiki, marafiki wasanii na hata wakenya waliamka na kupokea habari za kuhuzunisha kuwa msanii wa nyimbo za Ohangla Lady Maureen ameaga dunia ilhali hazikuwa habari za ukweli.

Msanii Esther Akoth almaarufu Akothee ameweka mambo wazi na kusema kuwa  yuko uhai na kuwaimiza wananchi wasifuatilie habari ambazo zimesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Akothee ambaye amekuwa rafiki wa karibu wa Lady Maureen katika safari yake ya uponyaji aliposti picha na kukana madai hayo.

Pia aliposti picha ambayo shabiki wake mmoja alisema kuwa ameaga dunia, hii ni njia ya kuambia wananchi kuwa mitandao ina nguvu ya kuuwa mtu yeyote ilhali yuko hai.

"LADY MOURINE IS STILL ALIVE 🙏🏾 I hope this is not the Akothee I am thinking of , IF its Akothee your Auntie or your sister then ,my condolences poleni

I know there could be so many akothees dying un noticed , If any of your relatives die ,who has the same name as me, please ,Put both Names ON your posts , stop shocking my relatives R.I.P. ESTHER AKOTH KOKEYO ( AKOTHEE ,MADAMBOSS , SUMBUA TAARIF ,NYAR AJOS TINGA , THE MOTHER OF FIVE." Akothee alinena.

Habari hizo zilienea sana jumatano kwenye mitandao ya kijamii isha baadaye ikasemekana aliye aga dunia ni msanii Maureen Nyar Awendo bali si Lady Maureen.

Maureen amekuwa kwenye matibabu kwa miaka miwili sana baada ya kupatikana ana upungufu wa damu mwilini ni hali iliodhoofisha afya yake sana.

Mama yake akizungumza alisema kuwa Lady Maureen yuko hai na anaendelea kupokea matibabu.

“Lady Maureen ako hai na mzima. Amegonjeka lakini yupo Mzima. Ata sisi tumeshanga kuskia ati ameaga."

Mapema mwaka huu msanii Akothee alijitokeza na kumsaidia Maureen kwa kulipa gharama na hospitali na hata kumjengea nyumba.

Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia kupona kwa haraka.