Lahaula! Jamaa auawa na mpenzi na mwili kupakiwa katika gunia Meru

A crowd mills around the murder scene
A crowd mills around the murder scene
Kijiji cha Gitimbine kaunti ya Meru kimegumbikwa na wingu jeusi la simanzi mapema asubuhi baada ya Joel Kaberia, 45 kuuawa kinyama na mpenzi wake Bridget Gacheri ,22.

Soma hapa hadithi nyingine:

Joel alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa kuuza nyama katika vichinjio mji wa Meru na alikuwa anamiliki vichinjio viwili katika soko la Gitimbine. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, mzozo baina ya hawa wawili ulisababishwa na migogoro ya pale nyumbani.

Afisa kamanda wa polisi Imenti kaskazini James Githinji ameidokezea gazeti la Star kuwa maafisa wa upelelezi tayari wamemkamata mshukiwa na wanamhoji ili kubaini chanzo cha ugomvi uliosababisha mauti.

"Hatuna habari za kina kuhusu swala nzima. Tumeanzisha uchunguzi. Tumemkamata Gacheri ili kufanya uchunguzi wetu." amesema Githinji.

Soma hapa hadithi nyingine:

Maafisa wa upelelezi wamepata msumeno silaha ambayo ilitumika kumjeruhi na kumuua Joel. Wanandoa hawa walikuwa wameoana ndoa ya mwaka na nusu. Mwili wa mwendazake umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Meru Level 5.