Lampard ashutumu uongozi wa Premier league kwa kuanzisha msimu ujao mapema

Mkufunzi wa Chelsea ameshutumu vikali hatua ya usimamizi wa ligi kuu ya Uingereza wa kuanzisha msimu mpya wa mwaka 2020/2021 septemba 12 akisema asilimia kubwa ya wachezaji hawatakuwa na muda wa kupumzika baada ya kushiriki michezo ya mabingwa bara Ulaya na Uropa .

Chelsea watakuwa wakicheza dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wiki hili kwa awamu ya mkondo wa pili katika mechi za Champions league .Munich wanaingia katika mchezo huo wakiwa na  matumaini makubwa ya kufuzu kwa awamu ya robo fainali baada ya kushindi mkondo wa kwanza kwa magoli 3-0 ugani Stamford Bridge.

Lampard amesema kuwa kutokana na michezo hiyo inayoendelea,huenda asilimia kubwa ya wachezaji hawatakuwa na muda wa kupumzika kutokana na ratiba mpya wa EPL msimu mpya.

Wachezaji Cesar Azpilicueta, Christian Pulisic na Pedro watakaso kushiriki mtanange huo baada ya kujeruhiwa wakati ewa fainali ya kombe la FA Jumamosi dhidi Arsenal mechi waliyopoteza magoli 2-1 .