Wasichana pacha ambao waliunganishwa baada ya miaka 19 wakiishi na familia mbili tofauti lazima wafanyiwe tambiko kabla ya kuishi pamoja kama familia moja . Mahojiano na wazee kutoka jamii ya waluhya yameonyesha kwamba matambiko hayo ni ya kuzuia kurejelewa kwa tukio kama lililowasibu wasichana hao katika kizazi chao .
Matokeo ta DNA yaliyotolewa siku ya jumamosi yalionyesha kwamba Melon Lutenyo na Sharon Matias ni madada wa damu moja .wawili hao walilelewa na mama tofauti hadi walipokutana kupitia mitandao ya kijamii .Melon amelelewa na mamake mzazi Rosemary Onyango ilhali Sharon amelelewa na Angeline Omina mtaani Kawangware hapa Nairobi walipobadilishwa wakiwa katika shule ya chekechea .
‘Wazee lazima wamchinje kuku mweusi ambaye hajataga na kutayarisha dawa za miti shamba ambazo zitanyunyuzwa karibu na lango kuu la boma lao ili kumaribisha binti yao ambaye hakuwa nao kabla ya mlo wa familia nzima’,amesema Ndeta Chimasia anayeisitiza kwamba lazima kuku huyo awe mweusi .