Lazima nitembee miguu mitupu nikiwa Kenya - Jah Cure

Mkali wa Jamaica Jah Cure amekiri kuwa kinyume na wasanii wengi mashuhuri ambayo hutembea humu nchini, yeye yupo tayari kuungana na wakenya na kutangamana nao hadi katika ghetto za Kibera.

Isitoshe, msanii huyu wa vibao kama vile, before I leave, ameapa kuwa lazima atatembea akiwa miguu tupu kama mojawapo ya kushirikiana na utamaduni wa ki Afrika.

Jah Cure yumo nchini kwa siku kadhaa ambapo anapaniwa kuwatumbuiza wakenya katika tamasha la Umoja splash, katika bustani la Uhuru, Nairobi Jumamosi.

"Nataka nishirikiane na wakenya kwani sikuja Afrika kuimba pekee, naweza tembea miguu tupu wiki hii ili nihisi nchi kavu ndio nijihusishe na watu." Alisema Jah Cure katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta pindi tu ndege yake ilivyo tua.

Aliongeza,

Nataka kwenda kuona jamii ya Maasai kisha nivalie kama wao.

Alipoulizwa afichue kile ambacho wakenya watatarajia kutoka kwake siku ya Jumamosi msanii huyo wa Lovers rock aliwahakikishia wakenya kuwa atatumia nguvu zake zote atakapofika katika jukwaa.

Ntaimba kutoka moyoni mwangu, nitaimba kila wimbo ambao mwajua na pia nyimbo ambazo mtaitisha kwa sababu moyo wangu umejawa na furaha na sababu Kenya kunafaa mno. 

Jah Cure ambaye mwisho kutembea Kenya ilikuwa miaka miwili iliyopita, anahuzunika kwa kuwa hakuweza kuja tena kabla ya mwaka huu lakini ana furaha kuwa aliwasili salama salmini.

Nataka kuhisi upendo wa wakenya na nataka kukutana na ndugu zangu kwani umekuwa mda mrefu. 

Nahisi vibaya kwano ningefika humu mapema kwani umekuwa mda mrefu lakini namshukuru mola nimefika salama.

Niko tayari kutangamana na wakenya kutoka Kibera kwani nilitembelea maeneo hayo. Niko tayari kutembea tena kwani napenda kuona watu wangu.