Lebo ya WCB yang'ara nyimbo 4 bora afrika mashariki 2019

Diamond-696x395
Diamond-696x395
Idadi ya nyimbo nne za wasanii wa lebo ya WCB zimeshika nafasi za kwanza katika orodha ya nyimbo kali zilizoteka anga mwaka wa 2019.

Shirika la habari la BBC lilichapisha orodha ya nyimbo 10 bora kutoka Afrika mashariki.

https://www.instagram.com/p/B6mdvOxntK2/

Hii ina maana kuwa lebo ya Diamond Platnumz ina wasanii ambao wamejitahidi pakubwa kurekodi nyimbo zinazowakonga nafsi mashabiki wengi.

Nyimbo hizi pia zimepata upigwaji mkubwa katika redio na runinga kubwa hapa eneo la afrika mashariki.

Haya yanajiri huku kituo cha habari cha CNN kimeorodhesha Diamond Platnumz kama staa mkubwa Afrika.

Diamond amekuwa katika mstari wa kwanza kuupeleka muziki wa Afrika katika levo za kimataifa.

Kando na kuwa msanii, Simba ana mchango mkubwa sana katika jamii.

Lebo ya WCB imeweza kuwasimamia wasanii wengi na kuwafanya mastaa wakubwa Afrika Mashariki.

Wasanii hawa ni Rayvanny, Mbosso, Dadake Queen Darleen, Lava Lava.

Rich Mavoko na Harmonize walikuwa mastaa katika lebo hii na baadae kuitema na kushughulika na muziki wao.