Legalize it! Waziri wa fedha atoa wito wa kuhalalisha bangi

Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Tito Mboweni ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuhalaliisha biashara ya bangi ili kuongeza ukusanyaji ushuru.

Alitoa pebdekezo hilo katika Twitter yake na kuongeza kuwa atawasilisha wazo hilo katika kikao cha baraza la mawaziri

Pia liweka picha inayoonesha mmea huo unavyokuwa:

Uuzaji wa bangi ya kiasi chochote ni kinyume cha sheria, kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini.

Je unazifahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa?

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa, kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi.

Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchini Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.