Leo mfalme amezaliwa! Diana Marua aonesha sura ya mwanawe 'Majesty'

Siku ya Jumatano, majira ya saa saba na dakika nne mchana, Bahati na mkewe Diana Marua walimkaribisha mtoto wao wa pili pamoja kwa jina Majesty Bahati katika hospitali ya RFH hapa mjini Nairobi.

Babaye Majesty, Bahati alikuwa wa kwanza kumkaribisha mwanawe Majesty duniani huku akimshukuru mola kwa zawadi hiyo mpya kupitia mtandao wake wa kijamii.

Masaa kadhaa baadaye, mkewe Diana Marua alitumia mtandao huo huo kuonesha sura ya mwanawe kwa mara ya kwanza.

Diana aliandika,

They call me Mama Morgan, Mama Heaven and Today, My King has been Born 💃 Wednesday 14. 08. 2019 at  at exactly 1:04pm MAJESTY BAHATI 👑 weighing 3.5kgs 😍 GLORY TO GOD 🙏 WELCOME  

Tazama picha ifuatayo,

Baada ya kuzaliwa, Majesty amepata ajira yake ya kwanza akiwa na umri wa dakika 30.

Hii ni baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa hospitali ya RFH. Wakenya wamezidi kumpa kongole Bahati mtandaoni huku wakichukua nafasi hio kumkaribisha Majesty Bahati ulimwenguni.