Leroy Sane atasaini mkataba wa miaka 5 na Bayern Munich

Winga wa Manchester City Leroy Sane atasaini mkataba wa miaka mitano na Bayern Munich. Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 24, hatakuwa mchezaji mwenye kulipwa kiwango cha juu zaidi katika ligi ya Ujerumani. (Bild)

Everton iko tayari kumtafuta nahodha wa Paris St-Germain Thiago Silva, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa Juni. Timu ya awali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, 35, AC Milan pia imeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Le10Sport)

Upande mwingine Arsenal inapania kumsajili mshambuliaji wa Norwich City, Max Aarons, 20, lakini haiko tayari kulipa £30m. (Goal via Norwich Evening News)

Manchester City imewasiliana na Barcelona kuhusu mshambuliaji Sergi Roberto. Lakini mchezaji huyo wa Uhispania, 28, ataondoka Nou Camp ikiwa tu klabu hiyo itamuarifu kwamba sasa anaweza kuhamia kwingineko. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Kiungo wa kati wa Newcastle United, Matty Longstaff, 20, huenda akaishia katika mahasimu wao wa Ligi ya Primia Watford ikiwa atafikia makubaliano ya usajili na klabu ya Italia.

Inter Milan inaweza kufikiria uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wa Slovakia Milan Skriniar, ambaye amehusisha na Manchester City, ikiwa tu watapokea pendekezo la kumuuza mchezaji huyo kwa zaidi ya thamani ya €80m. (Tuttosport via Manchester Evening News)

Manchester United imeanza majadiliano na klabu ya Argentina Velez Sarsfield ikiwa na nia ya kumsajili kiungo wa kati Thiago Almada, 19, ambaye katika moja ya kipengee chake anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa malipo ya £20m ambaye pia amehusishwa na kuhamia Arsenal. (Fichajes, in Spanish)

-BBC