MY LIFE WAS IN DANGER:Babu Owino azungumia Kilichotokea B Club

Mbunge wa Embakasi mashariki Babu owino ametuma taarifa kuhusu tukio la jana ambapo anadaiwa kumjeruhi mtu mmoja kwa kumpiga risasi .Babu amesema  maisha yake yamekuwa hatarini na jana ilikuwa kilele cha jaribio la wapinzani wake kumwangamiza na walimzingira alipokuwa na rafiki zake katika eneo la B club . Amesema  uchunguzi unafaa kufanywa ili kubaini kilichotokea na  juhudi za wapinzani wake hazitomfanya akome kumwunga mkono rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila odinga.

Katika taarifa yake ,Owino amesema aliandikisha taarifa na polisi kuhusu vitisho alivyopokea kuhusu kaisha yake  katika kituo cha polisi cha Bunge tarehe 17 mwezi novemba mwaka jana .Amesema polisi wanafaa kufanua uchunguzi huru na bila woga  na ukweli kuhusu kilichofanyika utajulikana . Ameongeza kuwa amekuwa akiishi chini ya hofu ya kutishiwa kisiasa na wapinzani wake .