Ligi ya Uingereza: Man City wataweza kutetea taji lao?

Klabu ya Manchester City hii leo watakuwa wanachuana na Newcastle uwanjani St James Park.

Pep Guardiola ambaye ni mkufunzi wa City ana matumaini kuwa vijana wake bado wanaweza kutetea taji hilo kwani kwa sasa City wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 28 nyuma ya Liverpool na Leicester ambao wako na pointi 37 na 29 mtawalia.

 Newcastle kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 14 huku wakiwa na pointi 15.

Mechi zingine zitakazochezwa hii leo ni;

Liverpool vs Brighton

Burnley vs Crystal Palace

Chelsea vs Westham

Tottenham vs Bounermouth