Ligi ya Uingereza: Mechi kali ya kutazamwa wikendi

Ligi ya Uingereza itakuwa inasakatwa hii leo baada ya mapumziko mafupi ya juma moja. Klabu mbalimbali zimejiandaa vilivyo ili kuhakikisha kuwa wikendi hii wataandikisha ushindi.

Wikendi hii ni ya kusisimua kwani mechi kali zaidi itakuwa Manchester City dhidi ya vijana wake Frank Lampard Chelsea. Kumbuka Pep Guardiola ambaye ni mkufunzi wa Mancity aliweza kuadhibiwa vikali na Liverpool kule uwanjani Anfield kwa kunyukwa mabao tatu kwa moja.

Ni kichapo ambacho kilichangia klabu ya City kushushwa daraja hadi nambari nne katika ligi hiyo wakiwa na pointi 25.

Chelsea kwa upande wao wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 26 baada ya kuandikisha ushindi katika mechi yao dhidi ya Crystal Palace.

Je, nani mkali zaidi? Mancity ama Chelsea? yote hayo yatathibitishwa wikendi hii.

Mechi nyingine ya kutazamiwa wikendi hii ni ya klabu ya Tottenham ikichuana na Westham.

Si mechi kali vile lakini umuhimu wa mechi hiyo ni je, Jose Mourinho ambaye ni mkufunzi wa sasa wa Tottenham baada ya Mauricio Pochettino kupigwa kalamu ataweza kuandikisha ushindi wake wa kwanza na klabu hiyo?

Kumbuka Tottenham kwa sasa wanashikilia nafasi ya 14 wakiwa na pointi 14 huku mashabiki wa klabu hiyo wakiwa na matarajio kuwa Mourinho atachangia pakubwa kurudisha makali ya klabu hiyo.

 Mechi zingine ambazo zitachezwa wikendi hii ni;

Arsenal vs Southampton

Brighton vs Leicester

Crystal Palace vs Liverpool

Sheffield United vs Manchester United