Ligi ya Uropa: Man United na Arsenal wataweza kuandikisha ushindi?

Raundi ya tano ya Ligi Uropa itakuwa inachezwa leo huku wakufunzi wa klabu mbalimbali  wakitarajia  kuandikisha ushindi ili wafaulu kuendelea katika ngazi utakaofuata baada ya michuano ndani ya vikundi.

Astana vs Manchester United

Klabu ya Astana itawakaribishwa vijana wake Ole Gunnar Solsjaer nyumbani kwao Astana Arena.

Katika kundi hilo, Astana wanashikilia nafasi ya nne bila pointi kwani hawajaweza kushinda mechi hata moja, huku Man United wakiwa kileleni na pointi 10.

 Wikendi iliyopita katika ligi ya Uingereza, Man United walitoka sare ya bao tatu dhidi ya Sheffield United. Je, leo wataandikisha ushindi? Yote hayo yatathibitishwa leo.

Arsenal vs Eintracht

Ni mchuano ambao utashindaniwa uwanjani Fly Emirates.

Arsenali wanashikilia nafasi ya kwanza katika kundi hilo wakiwa na pointi 10, huku Eintracht wakiandikisha pointi 6 katika nafasi ya tatu.

Unai Emery ambaye ni mkufunzi wa Arsenali ana matumaini kuwa vijana wake wataweza kushinda.

 Kumbuka wikendi iliyopita Arsenali waliponea chupuchupu kupigwa na Southampton baada ya mechi hiyo kukamilika sare ya mabao mawili.