Lipa deni!' Wakenya wamwambia Daddy Owen baada ya kushtakiwa na Sarkozi kwa udanganyifu

Kwa muda sasa, sanaa ya nyimbo za injili imekuwa na matatizo na mshikemshike baina ya wasanii wenyewe si kutoka kwa Ringtone mpaka kwa Bahati.

Wote wamekuwa wakienea katika mitandao kwa mambo yote mabaya,bbadala ya kuonyesha mfano mwema kwa mashabiki wao na wasanii chipukizi.

Daddy Owen ameshtakiwa na msanii mwenzake Reagan Sarkozi aka Mwana wa Nzambe kwa kutomlipa kazi aliomfanyia huku akidai anamdai millioni mbili.

Alidai kuwa alimwandikia wimbo wake wa 'vanity' ilhali hakumlipa chochote.

Msahabiki na wekenya baada ya kuona vita hivyo walimwambia Daddy Owen alipe deni lake, haya hapa baadhi ya maoni ya wakenya.

careen_de_generes Hadi kwenye mitandao 2much watu wa Mungu

_waswa 😂😂😂😂mlikua mnaingilia willy Paul eti alihamia secular but see your gospel artists… Lol

elvis_popo 😂😂😂lakuni zzzady Owen pia wewe ni fire unarusha hawa ma boy wako a good one… Kwanza Ule msee kipofu cjui deno ukamkula ma doe sasa pia huyu batoto ba Congo.. Mwana wa zambe.. 😂😂

nats__nana @daddyowen dawa ya deni ni kulipa,mpe mwenzio haki yake jamani

kaplotimwenyewe Sad kuona msanii mwenzako akikutendea ya Musa na firauni..huku akisema ni Mwokovu😏

Kupitia mtandao wa kijamii, Reagan alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na suala hilo.

 ‘Nilishughulikia  nyimbo  hizo pamoja na melody  Pitson  hawajui watu katika wimbo huo. Daddy Owen tafadhali nipe  jibu kuhusu pesa zangu.’ Anasema