Sekta ya benki nchini imekuwa ikibadilika kila kuchao. Kutoka enzi zile wakati watu walikuwa wakisubiri kuhudumiwa kwa mrefu hadi nyakati za sasa ambapo unaweza kufanya shughuli zako za benki kwa simu ya mkononi.
Benki nchini Kenya zimekuwa zikiorodheshwa kuambatana na umiliki. Baadhi ya benki zinamilikiwa wawekezaji wa kibinafsi na kampuni za humu nchini huku zingine zikimilikiwa na watu binafsi au mashirika ya kigeni.
Benki nyingi nchini zina akaunti za amana ya kudumu (fixed deposit accounts). Hata hivyo kila benki ina masharti na vigezo kuhusu viwango vya chini vya pesa unazohitaji ili kupata huduma ya akaunti ya Amana ya kudumu na faida ambayo pesa hizo zitazalisha.
Hii ni orodha ya benki ghali mno nchini Kenya.
Kenya Commercial Bank
Equity Bank
Faulu Microfinance Bank Ltd
I &M Bank Ltd
Barclays Bank
Standard chartered Bank
CFC Stanbic Bank
National Bank of Kenya
Kenya post savings Bank
NIC Bank
TAARIFA IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO