Orodha ya kampuni zinazomilikiwa na Uhuru Kenyatta unazostahili kujua

Uhuru.Kenyatta.family
Uhuru.Kenyatta.family
Uhuru Kenyatta ni rais wa nne wa Kenya. Amekuwa rais tangu mwaka 2013.

Ni wazi kwamba familia ya Kenyatta in tajiri sana.

Tuangazie baadhi ya kampuni zinazomilikiwa na na familia ya Kenyatta.

Heritage Groups of Hotels

Baadhi ya maeneo ya kustarehe na hoteli chini ya kampuni hii ni kama ifuatavyo :

Great Rift Valley Lodge

Yapendwa sana kwa mikutano ya kisiasa na ina uwanja wa gofu wenye mashino 18. Inapatikana katika eneo la Naivasha

Usiku mmoja katika hoteli hiyo utakugharimu kati ya shilingi 30,000 na Ksh150,000 kulingana na huduma unazotaka.

Kipungani Explorer

Ina jumla ya matawi 13 katika kisiwa cha Lamu. Chumba cha bei nafuu sana katika hoteli hiyo kitakugharimu shilingi 115,000.

Mara Explorer

Yapendwa sana na wapenzi wa kutalii pori, Mara explorer inapatikana katika Mbuga ya wanyama ya Maasai Mara.

Usiku mmoja katika hoteli hiyo utakugharimu shilingi 60,000.

Commercial Bank of Africa

Benki hii pia inaendesha shughuli zake nchini Uganda na Tanzania. Inamiliki mali ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 100. Miaka michache iliyopita pia ilizindua huduma ya akiba na mikopo kupitia kampuni ya mawasiliano ya Safaricom na M-Shwari.

Brookside Dairies

Mwaka 2013.  Brookside ilitwaa umiliki wa kampuni ya maziwa ya Molo kwa kima cha shilingi bilioni 1.1 na kuongeza upana wa soko lake la maziwa nchini Kenya hadi asilimia 55.  Hatua hiyo ilipigwa jeki pia na kuanzishwa kwa kituo cha kuhifadhi maziwa mjini Narok chenye lita 1,500.  Brookside pia inamiliki viwanda vya maziwa vya Ilara, Delamere na SpinKnit (Tuzo).

Ukulima umiliki wa mashamba makubwa ya Kahawa, majani chai na mkonge katika maeneo ya Kati, Bonde la Ufa na eneo la Pwani.

Elimu ,  Shule za Peponi, msururu wa shule za kimatifa, huku kila mwanafunzi akilipa takriban shilingi  620,000 kwa muhula kwa wanafunzi wa malazi.

Enke limited, Kampuni inayoendesha biashara mbali mbali zikiwemo majumba na maeneo ya makaazi.

Vyombo vya habari  Mediamax Group, inayomiliki K24 TV,  Gazeti la the people, Kameme Fm, Meru Fm na milele Fm.

Taarifa imetafsiriwa na Davis Ojiambo