Liverpool waongeza uongozi wao kileleni baada ya kuinyuka Wolves

wolves
wolves
Bao la dakika za lala salama la Roberto Firminho liliwasaidi Liverpool kuwalaza Wolves mabao 2-1 na kuongeza uongozi wao kileleni mwa jedwali kwa alama 16.

Nahodha wa the Reds Jordan Henderson alianza kufunga kutoka kwa kona ya Trent Alexander-Arnold baada ya dakika nane lakini Wolves wakasawazisha dakika sita baada ya mapumziko wakati Raul Jimenez alipofunga.

Inter Milan wamemsajili wing'a wa Chelsea Victor Moses kwa mkopo kwa muda wa msimu uliosalia huku kukiwa na uwezekano wa mkataba wa kudumu. Raia huyo wa Nigeria alianza tajriba yake Crystal Palace na kuhamia Wigan kabla ya kujiunga na Chelsea mwaka 2012. Ameshinda ligi ya Uropa, Primia na kombe la FA na kuchezea Liverpool, Stoke na West Ham kwa mkopo.

Moses alijiunga na Fenerbahce kwa mkopo Januari mwaka 2019, akiwa hajachezea Chelsea tangu Oktoba 2018. Inter pia walimsajili Ashley Young kutoka Manchester United mapema mwezi huu.

Manchester United na Sporting Lisbon bado hawajakubaliana kuhusu uhamisho wa Bruno Fernandes. Zikiwa zimesalia siku nane kwa dirisha la uhamisho kufungwa, mkataba huo umekwama huku kukiwa hakuna majadiliano mapya yamepangwa.

Wiki iliyopita, United walikua wana matumaini ya kukubaliana mkataba kumnunua kiungo huyo wa kati wa umri wa miaka 25. Inadaiwa kuwa mkataba wa Fernandes unajumuisha kipengee kuhus ajenti wake ambacho ndio kinatatanisha.

Chelsea imetoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, kwa mkopo, hadi mwisho wa msimu huu. Babake Cavani amesema nyota huyo atajiunga na Atletico Madrid ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itaafikiana na PSG. Kwingineko Tottenham wanamlenga mshambuliaji wa Real Sociedad, Mbrazil Willian Jose na kiungo huyo wa miaka 28 anatarajiwa kusafiri London kwa mazungumzo.

Barcelona wamemuulizia Christian Eriksen kwa lengo la kumsajili kutoka Tottenham katika dirisha la uhamisho mwezi huu. Eriksen alikutana na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy jumanne na kusisitiza kua anataka kujiunga na Inter Milan mwezi huu. Inter wanamng'ang'ania lakini sasa inaonekana kuwa Barcelona wameingia katika kinyang'anyiro cha saini yake.

Hata hivyo bado hakuna mktaba kati ya Tottenham na Inter kuhusu ada ya Eriksen.

Jukwaa liko tayari kwa tuzo za mwaka huu za SOYA zinazoandaliwa mjini Mombasa. Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga analenga kutwaa tuzo la mwanaspoti wa mwaka atakapokutana na Timothy Cheruiyot, Conseslus Kipruto, Geoffrey Kamworor na bingwa wa dunia wa Marathon Eliud Kipchoge.

Wakati huo huo Evelyne Okinyi anawania kujinyakulia tuzo la kinadada na atapambana na Hellen Obiri, Ruth Chepng’etich, Beatrice Chepkoech na Brigid Kosgei.