Liverpool yawabwaga Chelsea 5-4 na kutwaa taji la Super Cup

adrian
adrian
Liverpool jana ilishinda Super Cup kwa mara ya nne katika historia yake kwa kuwanyuka Chelsea 5-4 kupitia mikwaju ya penalti. Pande zote mbili zilitoka sare ya 2-2 katika muda wa kawaida na wa ziada.

Wakati wa mikwaju hio, kipa Adrian alizuia mkiki ya Tammy Abraham na kupelekea ushindi wa mabingwa hao wa Champions League. Ushindi huu unajiri miezi miwili tu baada ya Jurgen Klopp kushinda taji lake la kwanza kama meneja wa Liverpool.

Chelsea wanafuatilia kinachoendelea na Manchester City kwa makini baada ya mabingwa hao wa ligi ya Primia kukwepa marufuku ya uhamisho kwa kukiuka kanuni za kuwasajili wachezaji wa chini ya miaka 18.

City walitozwa faini ya pauni elfu 315,000 lakini hawakupigwa marufuku baada ya FIFA kuwa walikiri makosa. Chelsea wakati huo huo walipigwa marufuku ya mwaka mmoja ya kusajili wachezaji na kutozwa faini ya pauni elfu 460 mwezi February, na wako katika mchakato wa kupinga marufuku hio kwa sasa, katika mahakama kutatua kesi za spoti.

Wamedinda kutoa taarifa yoyote lakini wanafuatilia jambo hilo kwa makini.

Barcelona na Real Madrid wamewasilisha ofa kwa Paris St-Germain kumtaka Neymar lakini zimekataliwa. Klabu ya zamani ya Neymar Barcelona wanaaminika kutoa ofa ya Uro milioni 100 pamoja na Philippe Coutinho.

Ivan Rakitic pia alijadiliwa kama sehemu ya mkataba huo. Real wamewasilisha ofa inayohusisha pesa na vilevile Gareth Bale na James Rodriguez. PSG walikuwa wanamtaka Vinicius Junior lakini Real haikuweka jina lake kwenye mkataba huo.

Inaaminika kuwa PSG wangependelea kumuuza Neymar kwa Real.