Is Love Blind? Wengi wanataka kujua kilichomvutia marehemu Tecra Muigai kwa Omar Lali

Bintiye  mmiliki wa Keroche Breweries Tecra Muigai amekuwa  katika ndimi za wengi na katika vichwa vya habari baada ya kifo chake  na kutolewa kwa picha ya mpenzi wake  Omar Lali .

Wengi na hasa mitandaoni  wameshindwa kufahamu kilichomvutia  msichana huyo kwa Lali ambaye kwa mujibu wa picha zinatolewa na mtindo wa maisha yake hakuwa mtu mwenye mwelekeo wa kistaarabu. Kando na madai yanayoibuka ya ulevi, raha kupindukia na utumizi ya dawa za kulevya, Lali  sasa anajipata katika mkondo mbaya wa sheria kwa kutoa taarifa zinazokinzana kuhusiana na hali iliyosababisha kifo cha mpenzi wake Tecra .

Hadi sasa mengi kumhusu marehemu Tecra hayajajulikana kwa sababu aliishi maisha ya usiri kinyume na dadake Anerlisa Muigai ambaye wengi wanamfahamu kutokana na  mtindo wake wa kusimulia maisha na shughuli zake katika mitandao ya kijamii. Tecra Muigai  aliaga dunia Mei tarehe 2  katika hospitali moja Nairobi ambako amekuwa akipokea matibabu tangu alipoanguka kwenye stairs huko Lamu alikokuwa na Lali .

Kulingana na gazeti la The Star, Lali na Tecra walikutana mwaka jana  na Aprili mwaka huu, Tecra alimtembelea Lamu ambako anaishi. Walikodi chumba katika hoteli ya Manda Diamond kisha baadaye wakahamia katika nyuma ya kujivinjari –ili kuwa  na muda wao binafsi mbali na macho ya umma.  Wakati  Tecra alipoanguka na kujeruhiwa, wazazi wake walimleta jijini kwa ndege ili apate matibabu hadi wakati alipoaga dunia. Duru zaarifu kuwa  uchunguzi wa mwili wake umeahirishwa huku makachero wakijaribu kuunganisha matukio na hali iliyopelekea kifo chake .

Picha ya nyumba ya Omar  iliyosambazwa mitandaoni imezua mhemko kweli .

Jarunda Mambobiad Unaacha residence unaenda omuresidence

Lucia Mendez Garzia Some want maisonettes others just want peace.

Nicholas Mijwang’a Hii ndiyo ‘private residence’?

Vicky Willi Beautiful mansions await us in heaven

Joseph Onyimbo Rich women love from their heart but broke women love the money they are seeing

Lilian Thurgood In Mombasa these are some of the best houses

Asher Omondi  This is the cottage they rented??

Marck Sang This house is good yawaa! Just because you were lucky to have a better house doesn’t give you the right to denigrate those that have humbler abodes.

Dennis Nyagowa Love is so strange. I had a niece who was a medical lecturer, she fell so much in love with her garbage collector. We couldn’t stop her. She died.

Marck Sang This house is good yawaa! Just because you were lucky to have a better house doesn’t give you the right to denigrate those that have humbler abodes.