Lukaku kujiunga na Inter Milan, Luiz ataka kuhamia Arsenal

lukaku
lukaku
Kiungo wa Manchester United Romelu Lukaku anakaribia kujiunga na Inter Milan baada ya Inter kuwasilisha ofa mpya ya thamani inayokisiwa kuwa pauni milioni 77.

Ofa hiyo inajumuisha pauni milioni 65 za awali na pauni milioni 21 za marupurupu.

Ajenti wa Lukaku Federico Pastorello, yuko Uingereza kwa mazungumzo muhimu na United huku Lukaku akisalia Ubelgiji ambako amekua akifanya mazoezi na timu yake ya zamani Anderlecht. United walikua wakimtarajiwa mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 kuripoti Carrington Jumanne.

Mlinzi wa Chelsea David Luiz anataka kuhamia Arsenal. Kiuongo huyo wa The Blues alifanya mazoezi mbali na kikosi cha Frank Lampard jana. Kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery anasema anataka kumsajili kiungo wa kati kabla ya makataa ya leo na inaaminika kuwa Luiz yupo kwenye orodha yake, ingawaje hajawasilisha ofa rasmi ya kumtaka.

Chelsea hawataki kumwachilia Luiz kwenda Arsenal kutokana na marufuku yao ya kusajili wachezaji wapya hadi msimu ujao wa joto.

Hayo yakijiri, DC United wanajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, wanapojaribu kujaza pengo lililoachwa wazi na Wayne Rooney anayeelekea Derby.

Kwingineko Manchester United wameongeza juhudi ya kufikia mkataba na kiungo wa kati Tottenham Christian Eriksen. Eriksen hayuko katika mpango wa muda mrefu wa Mauricio Pochettino, Tottenham - na tayari amethibitisha kuwa anataka changamoto mpya.

Huko Uhispania, Real Madrid wanafanya mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu kumsajili Neymar. Kiungo huyo wa Brazil anaaminika kuiambia PSG kwamba anataka kuondoka msimu huu wa joto, akiwa alijiunga nao mwaka wa 2017, lakini miamba hao wa Ufaransa hawajapokea ofa rasmi.

PSG hawana uwezekano wa kumuuza iwapo hawataregesha pauni milioni 200 walizotumia kumnunua Neymar.